×

Corona: Mnajifungia, Ugonjwa Wenyewe Virusi? Tokeni Mkafanye Kazi – Video

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewashangaa baadhi ya wananchi wa mkoa huo waliofunga biashara zao kisha kujifungia ndani wakiogopa kuambukizwa ugonjwa wa covid 19 unasababishwa na virusi vya corona.

 

Makonda amesema hayo leo Jumamosi, Aprili 4, 2020 wakati akizungumza na wanahabari alipokuwa akikagua miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa na Serikali mkoani humo.

 

“Hainingii akilini na wala siwezi kuielewa ya kwamba sasa imefika hatua wananchi wa Dar wanajifungia nyumbani kusubiri Corona wanashindwa kutoka kwenda kufanya kazi ugonjwa wenyewe ni virusi wataalam wanasema haisambai kwa njia ya hewa.

 

“Ni ugonjwa wa ajabu ambao sijawahi kuona Duniani ambao hutakiwi kutoka kwenda kazini, nimepita hata Ilala baadhi ya watu wameamua kufunga maduka kwa sababu ya Corona hiyo nayo ni uzembe. Tumeingizwa kwenye hofu ya ajabu haijapata kutokea Duniani watu wanajifungia majumbani eti kisa Corona mtakufa na njaa tokeni kafanyeni kazi, tulichozuia ni uzururaji.

 

“Hatuwezi kuwa tumejifungia pahala, hata Mungu anatushangaa kweli tunajifungia pahala kusubiri ugonjwa alafu kuna watu wanasema serikali inadanganya kwenu kuna mtu amekufa na Corona?”

 

“Ndiyo maana leo nawafuatilia wakandarasi, sasa nimkute mkandarasi hayupo site kisa corona, kuna wapuuzi huko wanasema Serikali inadanganya idadi imeongezeka, kwenu kuna mtu amekufa na corona? Kuna mtu kwenu anaumwa corona? Hiyo idadi imetoka wapi?” amesema Makonda.

Leave a Comment