Mbunge wa Konde (CUF), Khatibu Said Haji, amemuomba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aingilie kati ikiwezekana kumchukulia hatua stahiki, Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati, Salama Aboud Talib aliyekataa kukaa karantini na kusababisha maambukizi ya watu wawili kwenye familia yake.
“Ndani ya siku tatu ameng’ang’ana kukaa hospitali ya Mnazi Mmoja matokeo yake akatolewa kwa nguvu baada ya kuona jambo hili limekuwa kubwa sana. Baada ya malalamiko makubwa ndio alikubali kuwekwa kwenye karantini.
“Alifanya hivyo kwa sababu ya kiburi cha madaraka yake . Lakini pia nimpongeze Makamu wa pilli wa Rais Zanzibar kwa kukubali kukaa karantini alipotoka nje ya nchi bila kulazimishwa.
“Huu ndiyo utu, huu ndio ubinadamu leo waziri huyu ni nani anayekataa uamuzi wa Serikali hata uamuzi wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Hatuwezi kumchekea mtu mheshimiwa Waziri Mkuu kwa sababu ni waziri ulichukulie hatua haraka,” amesema Khatib Said Haji.
