MJI mzito huu! Wakati watu wakiwa bize kujilinda na gonjwa la Covid-19, wiki hii mji ulitikiswa na video iliyodaiwa kuwa ni ya fumanizi. Eti, Sarah kamfumania mumewe Harmonize akiwa na modo, Nicole!
Video ambayo ilikuwa inaonesha giza tupu, ilisambaa kwa kasi huko Instagram ambayo ndani yake ilisikika sauti ambayo ilidaiwa kuwa ni ya Sarah alipomfumania Harmonize nyumbani kwa Nicole, Mbezi Beach jijini Dar.
Kama hiyo haitoshi, madai yalienda mbali zaidi kwani kuna vyanzo vingine vilisema tifu hilo lilikuwa si fumanizi, bali ulikuwa ni ugomvi kati ya Sarah na mama mkwe ambaye amekuja kutoka Mtwara kwa ajili ya kununua kuku wa kwenda kufuga, maajabu haya!
Lakini wakati hayo yakiendelea kutikisa huko Instagram, Nicole aliibuka na kukanusha vilivyo na kusema hakufumaniwa wala nini na kilichomweka karibu yeye na Harmonize ni video ambayo yeye amecheza kama video queen na si vinginevyo.
Meneja wa Harmonize, Mjerumani naye alikanusha vilivyo madai hayo na kusema wanaoeneza uvumi huo ni wale ambao wana nia mbaya ya kumharibia msanii wake.
STORI: MEMORISE RICHARD, RISASI
