×

Vitu 10 vya Kubadilisha Nyumba yako

NYUMBA ni sehemu muhimu ambapo panatakiwa kuwa pa tofauti na ofisi au sehemu nyingine yoyote ili kuleta mvuto.

Kuna vitu kumi mihimu ambavyo vinaweza kubadilisha nyumba yako na kuonekana yenye mvuto wa kipekee, soma hapa chini;

  1. SANAA UNAYOPENDA

Una kuta zisizokuwa na chochote? Zipambe na sanaa ili kuchangamsha nyumbani kwako ila badala ya kununua sanaa kwa bei nafuu, nunua sanaa yenye uhusiano na wewe (inaweza ikawa kwa rangi unayopenda, kwa mfano).

Badala ya kuweka sanaa ya uchoraji wa wanyama, tafuta picha inayoonyesha kitu ambacho kina umuhimu kwako.

Pia unaweza kuweka vinyago na hata vitambaa vinaweza vikawekwa ndani ya fremu na kupamba ukutani.

  1. PAKA RANGI UKUTANI

Kama unamiliki nyumba unayoishi au umepanga na mwenye nyumba ataruhusu, paka rangi ukutani. Rangi ziwe za kukuvutia kama nyekundu nzito, mchanganyiko wa rangi ya machungwa na brauni au chochote kile kitakachokufanya ujisikie vizuri.

  1. MAKABATI YA VITABU

Ingawa watu wengi wanatumia makabati ya vitabu kuhifadhi vitabu, pia unaweza ukazitumia kuweka vitu vitakavyowapa watu ufahamu juu yako.

Hata kama wewe siyo msomaji au huna vitabu vingi, unaweza ukapamba makabati yako ya vitabu na picha, zawadi ndogondogo na kumbukumbu mengine uliyokusanya.

Ila jaribu kuwa na vitabu viwili ambavyo unavipenda, tafuta vitabu vya gharama nafuu vya kusoma na kutumia kupamba hapa.

  1. MIMEA

Bahati nzuri Tanzania ina wauzaji wengi wa mimea, waliyo barabarani. Wanauza mimea na maua pamoja na zitaleta uchangamfu nyumbani kwako.

  1. VYOMBO VINAVYOENDANA

Moja kati ya vitu vinavyofurahisha ukiwa na nyumba yako ni kuweza kukaribisha wageni nyumbani. Ukiwa na vyombo maridadi vya kutumia ukipata wageni itakusaidia kujiamini ukiwa unakaribisha wageni nyumbani.

  1. GODORO NA KITANDA

Theluthi moja ya maisha yetu hutumika kitandani, kwa hiyo ni muhimu kuwa na godoro la maana nyumbani. Pia, kama godoro lako ni nzuri sana hutataka kutoka kitandani!

Kuongeza msisimko kitandani, nunua kitanda kitakachofaa mtindo wako. Pia hakikisha una mashuka na mito bora itakayokufanya utabasamu ukiwa umelala.

  1. KOCHI INAYOLETA FARAJA

Mara nyingi, watu wanafikiri kwamba lazima wanunue fenicha nyingi wakihamia sehemu. Sasa, utaishia kutumia pesa nyingi kwenye vitu usivyovihitaji na ambazo hutahitaji, ukifanya hivi.

Itaendelea toleo lijalo.

Je, ungependa kujua nini kuhusu nyumba yako? Tuma maoni kwa namba hii 0654 880 707

 

Leave a Comment