×

Waziri Atangaza Wagonjwa 2 Kupona Corona – Video

WAZIRI wa Afya,  Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, leo Aprili 07, 2020, amesema watu wawili waliokuwa wakitibiwa ugonjwa unaotokana na maambukizi ya virusi vya corona (Covid-19) jijini Dar es Salaam na Arusha, wamepona.

Ameyasema hayo wakati akikabidhi baadhi ya vifaa vya tiba ya ugonjwa huo ka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, na kuongeza kwamba:

“Takwimu za leo kutoka maabara kwa waliochukuliwa sampuli zinaonyesha hakuna maambukizi, kwa hiyo wagonjwa wa corona Tanzania wanabakia 24; yaani  Zanzibar 7 na Bara 17.”

 

Leave a Comment