×

Ronaldinho Apata Dhamana, Atoka Gerezani

NGULI wa zamani wa soka wa Klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Brazil, Ronaldinho Gaucho,  na kaka yake Assis Moreira wamepata dhamana na kutoka gerezani nchini Paraguay baada ya kukaa huko kwa siku 32.

 

Wamepata dhamana ya dola milioni 1.6 (Tsh Bilioni 3.7) baada ya awali kukataliwa  kwa hofu wangeweza kutoroka.

Pamoja na kupata dhamana hiyo Jaji Gustavo Amarilla ameamuru wawili hao kutolewa gerezani na kwenda kuishi katika nyumba/hoteli katika mji wa Asuncion wakiwa chini ya uangalizi maalum.

 

Ronaldinho ambaye aliwahi pia kuzichezea Paris Saint-Germain (PSG) na AC Milan walikamatwa na polisi akiwa kaka yake nchini Paraguay kwa tuhuma za kuingia nchini humo na Passport feki za Paraguay ambazo zinawaonyesha  kama raia wa nchi hiyo wakati ni raia wa Brazil.

 

Leave a Comment