RAIS wa Marekani, Donald Trump, ametishia kulipiza kisasi dhidi ya India endapo nchi hiyo itapiga marufuku mauzo ya dawa ya Hydoxy-chloroquine, Trump amedai dawa hiyo inaweza kutibu corona, lakini India ambayo ni mzalishaji mkuu wa dawa hiyo duniani imepiga marufuku dawa hiyo kuuzwa nje.
Trump amesema amezungumza na Waziri Mkuu wa India, Narendra Mod,i na kumwambia kuwa Marekani inataka izipate dawa za Hydroxy-chloroquine ilizoagiza kutoka India ili zisaidie kuwatibu wagonjwa waliokumbwa na virusi vya corona na kusema kitendo cha India kupiga marufuku dawa hizo kuuzwa nje hakikubaliki.
Dawa hiyo inatumika kutibu wagonjwa wa Malaria lakini siku za karibuni Trump amekuwa akiinadi kuwa inatibu corona ambapo tayari sasa hivi inafanyiwa majaribio kubainisha iwapo inaweza kutumika kutibu kwa uhakika ugonjwa wa Covid -19 unaosababishwa na maambukizi wa virusi vya corona.
