×

Kinyerezi Walichangamkia Betika, Waeleza Linavyowapa Mkwanja

MAPEMA leo Jumatano, Aprili 8,2020,  timu ya maofisa masoko ya Global Publishershers imetembelea maeneo ya Kinyerezi, Tabata migombani na maeneo mengine ya   Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuendelea kulinadi  Gazeti la Betika ambapo baadhi ya wadau  wa kubeti wameendelea kulisifia kwa ujio wake huo kutokana na linavyoendelea kuwanufaisha katika kujipatia pesa  kutokana na miongozo mizuri iliyopo ndani ya gazeti hilo ya namna bora ya kubeti.
Baadhi ya wasomaji wa gazeti hilo wamesema kuwa hawataliacha kulisoma gazeti hilo kutokana na kuwa mkombozi wao hususani kwenye masuala ya kubeti na wao kunufaika na mkwanja.
Betika hutolewa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18, linachapishwa na Kampuni ya Global Publishers na huingia mtaani kila Jumatano.
Gazeti hilo lenye kurasa 20 za rangi linalojihusisha na masuala ya betting na lotto, lina takwimu za ligi tofauti na matangazo mbalimbali ya biashara.
Baadhi ya wasomaji waliokutana na timu ya maofisa masoko ya Global Publishers, walizidi kulisifia gazeti hilo kwa kuwa mkombozi wao kila kona ya nchi na kurahisisha kwenye masuala ya michezo ya kubeti.
Gazeti hilo heshima yake imeendelea kukua siku hadi siku na sasa lina watangazaji wengi ambao wanatangaza biashara zao kupitia Betika kwa bei nafuu.
Wote wanaofanya kazi na Betika wanapata ofa ya kutangaziwa biashara zao kwenye mitandao ya kijamii ya Kampuni ya Global Publishers katika Instagram, Facebook, Twitter na Global TV Online.

Leave a Comment