×

Breaking: Wawili Wafariki na Corona Dar, Idadi Maabukizi Yafikia 32 -Video

Wizara ya Afya leo Aprili 10, 2020 imetoa taarifa juu ya uwepo wa wagonjwa wapya wa Corona watano Dar es Salaam na wawili Zanzibar hivyo waliothibitika kuwa na Corona Tanzania ni 32 kati ya hao watano wamepona, 24 wanaendelea vizuri na matibabu na watatu wamefariki.

“Tunasikitika kutoa taarifa ya vifo viwili vilivyotokea leo miongoni mwa wagonjwa wa corona ambavyo ni Mwanaume(51) Mtanzania mkazi wa Dar na Mwanaume (57) Mtanzania Mkazi wa Dar hivyo kufanya idadi ya vifo vya corona Tanzania kufikia vitatu”- Ummy Ally Mwalimu, Waziri wa Afya

Leave a Comment