×

Global Kuwatunuku Mawakala, Wauzaji Magazeti na Wasomaji

Muuzaji wa magazeti wa maeneo ya Salenda akionesha gazeti la Championi.

 

TIMU ya masoko wa Global Publishers ikiongozwa na Mkuu wa Idara hiyo, Antony Adam, leo Jumamosi, Aprili 11, 2020, imetinga mtaani na kukutana na wauza magazeti wa Kampuni hiyo katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam na kuwahamasisha kuhusu promosheni baab’kubwa ya baba lao.

 

Ofisa Masoko wa Global Publishers, Songoro Bilal, akizungumza na muuzaji wa magazeti wa eneo la Kisutu-Posta.

 

Akizungumza na wauzaji hao, Adam amewaomba wauzaji hao kuwahamasiah wanunuzi wa magazeti hayo kuhusu Promosheni ya Shinda Gari inayoendeshwa na Magazeti ya michezo ya Championi na Spoti Xtra yanayochapishwa na Global.

 

Ofisa masoko wa Global Publishers, Anthon  Adam (kushoto) akizungumza na baadhi ya wauzaji wa magazeti aliokutana nao eneo la Magomeni.

 

Adama amewaeleza kuwa wakati wa kukabidhi zawadi ya droo kubwa ambapo mshindi atapewa gari mpya aina ya Toyota Funcargo, vilevile wakala ambayo atakuwa na mauzo mengi atakabidhiwa pikipiki mpya na muuza magageti atakayeuza nakala nyingi zaidi atapewa zawadi ya Tsh 100,000/- taslim hivyo kila mmoja kuanzia msomaji wa gazeti, wakala na muuzaji (watakaoshinda) watapewa zawadi.

 

Mkuu wa kitengo cha masoko, Global Publishers, Anthon Adam (kulia) akikutana na i muuzaji magazeti eneo la Magomeni.

 

JINSI YA KUSHIRIKI
Nunua Gazeti la Spoti Xtra, kisha ukurasa huu wa pili unakutana na kuponi yenye maelekezo ya kushiriki bahati
nasibu hiyo. Jaza kuponi kama maelekezo yalivyo.

JINSI YA KUTUMA:
Mpe kuponi yako muuza magazeti aliye karibu nawe popote ulipo, au peleka kwenye Ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza Mori, Dar, au tuma kwa njia ya barua, Jishindie Gari, Global Publishers, S.L.P 7534, Dar es Salaam.
Kwa maelezo zaidi, piga simu no: 0717 020792 au 0672 324759. –

MASHARTI YA KUSHIRIKI:
Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd na watoto chini ya miaka 18 hawaruhusiwi kushiriki bahati nasibu hii.
Kuponi zitumwe kutoka nakala halisi ya gazeti, vivuli (fotokopi) haviruhusiwi. Mtu anaruhusiwa kutuma kuponi nyingi kadiri awezavyo ili ajiongezee nafasi ya kushinda.
Kuponi zote zitachezeshwa kwenye droo ya awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu.

 

 

Leave a Comment