×

Nyota Azam FC Wakwama Ghana

Razak Abalora.

WACHEZAJI wa Azam FC, Razak Abalora na Yakubu Mohamed wameshindwa kurejea nchini baada ya kukwama nchini Ghana kutokana na nchi hiyo ya Afrika Magharibi kutangaza hali ya tahadhari na kuwataka wananchi wote kukaa ndani.

 

Wachezaji hao walikuwa kwao Ghana kwa ajili ya mapumziko kufuatia Ligi Kuu Bara kusimama kwa muda.Akizungumza na Championi Jumamosi, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Azam FC, Zakaria Thabith amesema kuwa kutokana na ugumu huo hawajui ni lini nyota hao wanaweza kurudi nchini.

“Unajua hali ya maambukizi katika nchi ya Ghana imekuwa kubwa kiasi cha serikali kutangaza hali ya tahadhari kwa kuwataka wananchi wote kubaki nyumbani kwao.

 

“Tumewasiliana nao na wametuambia hata vituo vya kufanyia mazoezi vimefungwa, hivyo imebidi tuwatumie fedha kwa ajili ya kununua vifaa vya mazoezi ambavyo vitawasaidia kuendelea na mazoezi wakiwa ndani.

 

“Hatuwezi kufanya lolote kwani hata safari za ndege zimefutwa, tunasubiria kuona ni jinsi gani hali ya mambo inaweza kuwa baada ya janga hili kupita,” alisema Thabith.https://youtu.be/m5xqvz1T5nQ

Leave a Comment