×

Azam FC Watoa Neno Sure Boy Kutua Yanga

UONGOZI wa timu ya Azam FC, umesema kuwa hadi sasa hawajapokea ofa yoyote ya usajili wa Salum Abubakar ‘Sure Boy’ huku ukihitaji timu hiyo kufika mezani kama kweli inamhitaji kiungo huyo.

 

Sure Boy amekuwa akihusishwa kujiunga na Yanga ambayo hivi karibuni iliweka wazi mpango wa kusajili wachezaji wa ndani, yaani wazawa wa daraja A kama ilivyo kwa kiungo huyo.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin Popat, alisema kuwa kama kweli Yanga inamhitaji mchezaji huyo, basi wafike mezani kwa ajili ya kufanya mazungumzo kama walivyofanya kwa mchezaji, Ditram Nchimbi.

 

“Hakuna namna yoyote Yanga wataweza kumsajili Sure Boy bila kufika mezani kwa kuwa bado ana mkataba mrefu na sisi, hivyo nawashauri kama kweli wanamhitaji mchezaji huyo, wafike mezani tufanye nao maelewano kama tulivyofanya kwa Ditram Nchimbi, maana sijapokea ofa yoyote kutoka kwao.

 

“Kwa upande wetu, Azam hatujawahi kuwa na shida kwenye masuala ya kuuza na kununua wachezaji, hivyo kama kuna timu yoyote tofauti na Yanga inamhitaji mchezaji wetu waje mezani tuzungumze,” alisema kiongozi huyo.

MARCO MZUMBE | Dar es Salaamhttps://youtu.be/9dg3ipBXK98?t=4

Leave a Comment