×

Mtatiro Ataka Walinzi Mipakani Kupambana ya Corona – Video

MKUU wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Julius Mtatiro,  akiwa katika ziara kwenye mipaka mbalimbali ya Tanzania na Msumbiji  upande wa Tunduru, amewaasa walinzi wa mipaka na viongozi wa mipakani kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa wa corona.

Akiambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya pamoja na timu ya kupambana na Korona ya Wilaya katika kikao cha UJIRANI MWEMA, Mtatiro amewataka walinzi wa mipaka wanaotoka upande wa Msumbiji wasiwape vibali watu wasio Watanzania na wanaotaka kufanya hivyo wawaeleweshe takwa la karantini ya lazima ya siku 14.

 

Mtatiro ameeleza kuwa Watanzania wanarejea kutokea nchi za Msumbiji na Kusini mwa Afrika wanapaswa kuruhusiwa kuingia Tanzania maana wanarudi nyumbani, na kwamba wao pia watawekwa karantini ya lazima kwa siku 14 pia na watajulishwa wakifika Tanzania.

Amewataka pia walinzi hao wa mipaka watoe elimu na kufuata masharti yote yanayotolewa na serikali za kila nchi na wataalamu wa afya.

 

Mkuu huyo wa wilaya anaendelea na ziara kwenye vipenyo vya mipaka mbalimbali ili kuongeza elimu na kuchukua hatua za kiulinzi na kujilinda dhidi ya corona.

 

Idd M. Mohamed
Tunduru,
17 Aprili 2020.

 

View this post on Instagram

 

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Ndg. Julius Mtatiro ameendelea na ziara katika mipaka mbalimbali ya Tanzania na Msumbiji kwa upande wa Tunduru na kuwaasa walinzi wa mipaka na viongozi wa mipakani kuchukua tahadhari ya kujikinga na korona. Akiambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya pamoja na timu ya kupambana na Korona ya Wilaya katika kikao cha UJIRANI MWEMA, Mtatiro amewataka walinzi wa mipaka wanaotoka upande wa Msumbiji wasiwape vibali watu wasio watanzania na wataka kufanya hivyo wawaeleweshe takwa la karantini ya lazima ya siku 14. Mtatiro ameeleza, kwa watanzania wanarejea kutokea nchi za Msumbiji na Kusini mwa Afrika wanapaswa kuruhusiwa kuingia Tanzania maana wanarudi nyumbani, na kwamba wao pia watawekwa karantini ya lazima kwa siku 14 pia na watajulishwa wakifika Tanzania. Mtatiro amewataka walinzi hao wa mipaka watoe elimu na kufuata masharti yote yanayotolewa na serikali za kila nchi na wataalamu wa afya. Mtatiro anaendelea na ziara kwenye vipenyo vya mipaka mbalimbali ili kuongeza elimu na kuchukua hatua za kiulinzi na kujilinda dhidi ya Korona. Idd M. Mohamed Tunduru, 17 Aprili 2020.

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

Leave a Comment