×

Corona: Wenye Kipato Duni Kupatiwa Ruzuku na Serikali

RAIS wa Kenya, Uhuru Kenyatta, ametangaza hatua za kuwasaidia watu maskini nchini humo kutokana na janga la ugonjwa wa Covid-19 unaoambukizwa na virusi vya corona.

 

Akihutubia taifa hilo jana (Alhamisi) alisema serikali imeanza mpango wa kutoa fedha kwa familia zenye kipato duni kila wiki kuanzia jijini Nairobi.

 

“Tumeshazitambua familia maskini jijini Nairobi zitakazoanza kupewa msaada huo kila wiki kupambana na Covid-19.  Mpango huo ulianza jana na wahusika tayari wamepata fedha hiyo,” alisema rais huyo.

 

Hata hivyo, hakutaja kiasi cha fedha ambapo kila familia maskini  itapata.

Leave a Comment