MAZUNGUMZO iwapo Ligi Kuu ya Uingereza (Premier League) iendelee au la yanafanyika leo ambapo wiki mbili zilizopita kulikuwa na mkutano kuhusiana na suala hilo ikiwa ni pamoja na makato ya mishahara kwa wachezaji katika mazingira ya mlipuko wa janga la ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona.
Ligi hiyo kwa msimu wa 2019-20 ilisimamishwa kwa muda usiojulikana na hadi leo haijulikani itaanza tena lini.
Mwanzoni, ligi hiyo ilikuwa inatatizwa na suala la watangazaji wake kuhusiana na madai ya malipo yanayhofikia Pauni milioni 762 ambayo yatafikia kiwango hicho Julai 12 mwaka huu.
Hata hivyo, hofu hiyo imepunguzwa kidogo na kampuni ya Sky Sports and Co iliyosema itatafuta makubaliano nafuu zaidi badala ya kuwabana wateja wao ambao wanawapromoti.
Hata hivyo, kumekuwepo na madai kwamba tarehe hiyo irudishwe nyuma hadi Juni 30 kwani ndiyo tarehe ambayo wachezaji kadhaa wengi wenye mikataba inapoishia kwa msimu huu.
Jana, Alhamisi, timu kubwa sita — Manchester zote mbili, Liverpool, Chelsea, Arsenal na Tottenham — zilijaribu kutetea msimamo huo, lakini zilishindwa kutokana na kupunguka kuwepo kwa klabu moja zaidi ya kuufanya mpango huo usipite.


