×

Bunge, CCM, ACT Wazalendo Wamlilia Mama Rwakatare

Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai amesema amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mchungaji Getrude Rwakatare na Bunge kwa kushirikiana na familia ya marehemu inaratibu mipango ya mazishi.

Chama cha Mapinduzi CCM kimepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa za kifo cha ndg. Getrude Rwakatare ambaye amekuwa mbunge wa viti maalum mkoa wa Morogoro kwa tiketi ya chama cha mapinduzi.

 

“Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mhe. Rwakatare (Mbunge wa Viti Maalum CCM), natoa pole kwa wafiwa wote wakiwemo Familia ya Marehemu, Ndugu,Jamaa, Wabunge na Waumini wa Kanisa la Mlima wa Moto, Mungu awape moyo wa subira katika kipindi hiki”-NDUGAI

 

TAARIFA YA TANZIA Chama cha ACT Wazalendo imeeleza kwa kupokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mchungaji Getrude Rwakatare, kilichotokea leo jijini Dar es Salaam. Chama chetu kinatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki.

Leave a Comment