Katika kipindi cha Front Page, leo Aprili 20, 2020, wachambuzi wamechambua Mjadala kuhusu wauguzi na madaktari katika kipindi hiki kigumu cha mlipuko wa Ugonjwa wa Corona.
Aidha Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Faustine Ndugulile, amealikwa kuchangia mjadala huu ambapo pia ameelezea kwa undani kuhusiana na ugonjwa wa Corona na mikakati ya serikali ambayo mpaka sasa wameichukua.
