×

Miili ya Baba na Mdogo Wake Yazikwa Mwananyamala, Dar – Video

Miili ya Hamza Juma Omary na mdogo wake Ally Juma Omary, wanaodaiwa kuuawa na mtoto wa Hamza, Hosam Hamza, imezikwa leo Julai 19, 2026 katika Makaburi ya Ndugumbi, Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi, mtuhumiwa huyo alikamatwa tarehe 17 Julai 2026 majira ya saa 9:00 alasiri eneo la Makongo, baada ya kukutwa akiwa na kisu kilichokuwa na damu pamoja na nguo zilizokuwa zimechafuliwa damu.

Polisi walisema baada ya kukamatwa na kuanza kufanyiwa mahojiano katika kituo cha polisi, ilibainika kuwa miili ya marehemu ilikuwa imefukiwa kwenye shimo baada ya tukio hilo.

Uchunguzi wa Jeshi la Polisi unaendelea ili kubaini zaidi mazingira ya tukio hilo, huku mtuhumiwa akiendelea kushikiliwa kwa hatua za kisheria.

Leave a Comment