Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Mabula Daudi Mchembe kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuchukua nafasi ya Dkt. Zainabu Chaula ambaye ameteuliwa Kuwa Katibu Mkuu wa Mawasiliano.

