×

Diamond Kuchangia Kodi Ya Pango Kwa Kaya 500 Nchini

Staa wa muziki wa Bongo fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’  leo Aprili 25, 2020 amesema kuwa atachangia ‘kodi ya pango’ kwa kaya 500 nchini kwa ajili ya kupunguza makali ya kiuchumi wakati huu ambapo Watanzania wanapambana na ugonjwa hatari wa virusi vya Corona ulioikumba dunia nzima.

 

“Najua katika kipindi hiki cha Corona, mambo mengi hayajakaa sawa, hususani upande wa biashara, nyingi zimeshuka na kupelekea hali ya kifedha kuyumba na mambo kuwa kidogo magumu kwa wengi wetu, mimi ni miongoni mwa walio ndani ya janga hili” alisema DiamondPlatnumz.

 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram nyota huyo ameeleza kuwa taarifa na utaratibu zaidi utatangazwa siku ya Jumatatu juu ya namna kaya hizo 500 zitakavyopatikana na kuweza kupata msaada huo.

Diamond Platnumz anakuwa msanii wa kwanza nchini kujitokeza hadharani na kuweka bayana kuwa atawasaidia wananchi chochote wakati huu wa janga la mlipuko wa virusi vya corona  vyenye kusababisha homa kali ya mapafu yaani (COVID 19).

Leave a Comment