×

Washindi wa Droo ya Pili ‘Baba Lao’ Wakabidhiwa Vitita

Mkuu wa Idara ya Masoko ya Global Publishers, Anthony Adam akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi wa droo ya pili ya bahati Nasibu ya Baba Lao.

WASHINDI wa sita waliopatikana kupitia droo ya pili ya Jishindie Gari na Spoti Xtra, iliyofanyika hivi karibuni wamekabidhiwa zawadi zao leo Jumamosi, Aprili 25, 2020.

 

Washindi wawili kutoa mkoa wa Dar na Pwani,  Yassin Suleiman kutoka Kibaha, pamoja na Hassan Katau wa Dar, ambaye aliwakilishwa na ndugu yake Hassan Khatibu, walikabidhiwa zawadi zao katika ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza Mori Jijini Dar.

Mkuu wa Idara ya Masoko ya Global Publishers, Anthony Adam akimkabidhi zawadi mshindi wa droo ya pili ya bahati Nasibu ya Baba Lao, Mzee Yassin Suleiman.

 

Washindi wa mikoani nao walikabidhiwa zawadi hizo kupitia kwa mawakala wa Global Publishers ambao wapo nchi nzima. Washindi wengine ni Samson Kabuje wa Mbeya, Aloyce Mdolwa wa Mwanza, Mwinjuma Ngayama wa Tanga na Yuda Mrema wa Moshi.

Mkuu wa Idara ya Masoko ya Global Publishers, Anthony Adam akikabidhi zawadi Hassan Khatibu kwa niaba ya mshindi ambaye ni Hassan Katau.

Mkuu wa Idara ya Masoko ya Global Publishers, Anthony Adam ambaye alikabidhi zawadi hizo kwa washindi alisema: “Leo tunatimiza ahadi ya kutoa zawadi za droo ya pili kama ambavyo tuliahidi, sitaki kuwa muongeaji sana, nafikiri hawa waliokuja ofisini watazungumza wenyewe.”

Hassan Khatibu (kushoto) akizungumzia ushindi huo kwa niaba ya ndugu yake,ambaye ni mshindi , Hassan Katau.

Mwakilishi wa Katau, alisema: “Mshindi huyo kwa Sasa anafikiria ushindi wa gari mara baada ya kufanikiwa kushinda fedha hizi, ndiyo maana huku kanituma mimi, ili nije kuchukua fedha na kuwa shahidi wa ushindi wake kupitia magazeti ya Spoti Xtra, hivyo hata mimi nimeshangazwa kuona zawadi zinatolewa kweli wala siyo utani.”

 

Naye mzee Suleiman alisema: “Nilikuwa nashiriki bahati nasibu nyingi za Global toka zamani, lakini sikuwahi kushinda, kwahiyo nilivyopigiwa simu kuwa nimekuwa moja ya washindi wa Jishindie Gari sikuamini.”

Mzee Yassin akizungumzia ushindi huo mnono kwake.

“Nimekuwa mwanachama wa magazeti ya Global Publishers likiwemo Spoti Xtra, kwahiyo nashukuru kwa kushinda licha ya kuwa nilipopigiwa simu kuambiwa nimeshinda nilidhani ni matapeli, kuja kuchunuza kumbe kweli” alisema Mzee Yassin.

 

Washindi wote walifanikiwa kuondoka na kitita cha shilingi 50,000, pamoja na tisheti zenye nembo ya Chomoka na Gari Mpya na Championi. Mshindi wa jumla atandoka na gari mpya aina ya Toyota FunCargo yenye thamani ya milioni 10.

Mkuu wa Idara ya Masoko ya Global Publishers, Anthony Adam akiwa katika picha ya pamoja na washindi hao pamoja na zawadi zao.

JINSI YA KUSHIRIKI

Nunua Gazeti la Spoti Xtra, kisha fungua ukurasa wa pili ambapo utakutana na kuponi yenye maelekezo ya kushiriki bahati nasibu hiyo. Jaza kuponi kama maelekezo yalivyo.

 

JINSI YA KUTUMA:

Mpe kuponi yako muuza magazeti aliye karibu nawe popote ulipo, au peleka kwenye Ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza Mori, Dar, au tuma kwa njia ya barua, Jishindie Gari, Global Publishers, S.L.P 7534, Dar es Salaam.

Washindi wakionyesha mkwanja waliokabidhiwa.

MASHARTI YA KUSHIRIKI:

Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd na watoto chini ya miaka 18 hawaruhusiwi kushiriki bahati nasibu hii.

Kuponi zitumwe kutoka nakala halisi ya gazeti, vivuli (fotokopi) haviruhusiwi. Mtu anaruhusiwa kutuma kuponi nyingi kadiri awezavyo ili ajiongezee nafasi ya kushinda. Kuponi zote zitachezeshwa kwenye droo ya awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu.

Issa Liponda

 

Leave a Comment