×

Watanzania Wengine 4 Wakutwa na Corona Uganda

 

WIZARA  ya Afya nchini Uganda imesema Watanzania wengine wanne ambao ni madereva wa malori, wamethibitishwa kuwa na virusi vya corona nchini humo, na kufanya visa vya corona Uganda kufikia 79.

Kwa mujibu wa taarifa ya wizara hiyo, waathirika waliwasili nchini humo kupitia mpaka wa Mutukula na walikuwa miongoni mwa watu 1,989 waliofanyiwa uchunguzi .

Ijumaa iliyopita, Kenya na Uganda zilipitisha hatua zitakazofuatwa na madereva wa malori yanayovuka mipaka, ikiwa ni katika kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo miongoni mwa wahusika.

 

Leave a Comment