MAZIKO ya aliyekuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro na diwani wa Kata ya Kiwanja cha Ndege, Isihaha Sengo, yamesitishwa baada ya Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo, Ikaji Rashid, kudai marehemu alionesha dalili za #COVID19.
Mganga Mkuu huyo alifika nyumbani kwa marehemu jana mchana na kuwakuta ndugu na jamaa wakijindaa kwenda kuzika kisha kuwataka kusitisha zoezi hilo na mwili kupelekwa chumba cha kuhifadhia maiti kwa uchunguzi.
Mganga huyo alisema ofisi yake imepata taarifa kutoka hospitali aliyokuwa akitibiwa marehemu kwa mara ya mwisho kuwa kuna viashiria kwa marehemu kuwa na maambukizi ya #CoronaVirus.
Alibainisha kuwa sampuli zitachukuliwa na kutumwa katika maabara iliyopo Dar es Salaam kwa ajili ya kufanyiwa vipimo.
