×

Wagonjwa wa Corona Kenya Wafikia 374

WIZARA ya Afya Kenya imesema wagonjwa wengine 11 wa corona wameongezeka jana na kufanya jumla ya visa vya corona kufikia 374.

 

Taarifa hiyo imetolewa na Naibu waziri wa Afya Dkt. Rashid Aman ambapo amesema kuwa kati ya maambukizi hayo mapya 11, wawili ni watoto wa miaka mitatu.

 

Hata hivyo, licha ya maambukizi ya Covid-19 kuongezeka nchini humo, idadi ya waliopona pia imeongezeka na kufikia 124.

 

Katibu Mkuu (Utawala) wa Wizara ya Afya, Rashid Aman amesema katika Wagonjwa hao 11, saba wanatokea Nairobi na wanne wanatokea Mombasa

 

Amebainisha kuwa Wagonjwa hao wapya wenye miaka kati ya mitatu na 70 wamepatikana baada ya sampuli 589 kupimwa ndani ya saa 24 zilizopita.

 

Mchanganuo wa Visa; Homa Bay (1), Kajiado (3), Kakamega (1), Kiambu (5), Kilifi (9), Kitui (2), Kwale (1), Mandera (8), Mombasa (97), Nairobi (241), Nakuru (2), Siaya (2) and Uasin Gishu (1).

 

Aidha, Katibu huyo amewataka Polisi kuhakikisha kuwa kuingia na kutoka katika Kaunti za Nairobi na Mombasa kunazuiwa ili kuzuia kusambaa kwa #COVID19.

 

Wizara hiyo imefafanua zaidi kuwa, Baa zitaendelea kufungwa ila Migahawa na sehemu za chakula zitapewa nafasi ya kufunguliwa zikikidhi vigezo vilivyowekwa

 

 

Leave a Comment