×

Mastaa Walioizidi Ujanja Corona

KWA sasa taifa na dunia vimekumbwa na janga la Virusi vya Corona ambavyo vinasababisha ugonjwa wa COVID-19 ambao bado unaendelea kuenea kwa kasi na kusababisha vifo vingi.

 

Kazi nyingi zimesimama hasa kwa wasanii ambapo kwa sasa hawaruhusiwi kufanya matamasha kutokana na kuzuiliwa kwa mikusanyiko, lakini wapo ambao wamejua kuitumia fursa kwa kutengeneza kazi nzuri ambazo zimekuwa zikibamba hata katika kipindi hiki cha Corona.

 

Usanii si kuimba tu bali ubunifu, jitihada na kutumia akili yote katika kuhakikisha brand yako haishuki na bado unaendelea kusikika katika masikio ya mashabiki wako. Hapa nina orodha ya wasanii ambao wameonesha spidi ya hali ya juu na kuiovateki Corona kwa kutoa kazi kali.

 

HARMONIZE

Mwanzo alitoa original ya ngoma ya Bedroom na kufanya vizuri katika mtandao wa YouTube kwa kutazamwa na watazamaji zaidi ya milioni mbili ndani ya wiki tatu, lakini jamaa baada ya kukaa chini na kujitathimini, akaona ni bora afanye ubunifu ndipo alipokuja na kichupa cha Bedroom remix ambacho kimejaza mastaa kama Darassa, Rosa Ree, Country Boy, Billnass, Young Lunya na Baghdad ambapo kwa sasa inashika ‘trending’ namba moja na kutazamwa na watazamaji zaidi ya laki tano ndani ya siku mbili, hii ni kutokana na ubunifu alioufanya kwa kutumia sauti mbalimbali ambazo nazo zimekusanya mashabiki lukuki.

 

ALIKIBA

Kichupa kikali cha Dodo ambacho kiliachiwa Aprili 8, mwaka huu kutoka kwa bosi wa lebo ya Kings Music, kilishika trending namba moja kwa muda mrefu, ngoma hii ilitazamwa na watazamaji zaidi ya milioni 3 katika mtandao wa YouTube na kuzishusha ngoma kibao ndani ya saa 24 na sasa ina wiki mbili tangu imeachiwa mtandaoni.

 

ZUCHU

Zuchu ni msanii mpya ambaye amesajiliwa lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) hivi karibuni, ameweza kuungurumisha makali yake kwa kutikisa na ngoma yake ya Wana kutoka katika Extended Playlist (EP) yake iliyojaza ngoma karibu saba ikiwemo Gwaru, Hakuna Kulala, Ashua aliyofanya na Mbosso, Nisamehe, Mauzauza aliyofanya na mama yake mzazi Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa. Kwa spidi aliyoanza nayo, hakika anaonekana kufika mbali, kwani ana melodi ya kipekee na utamu wa sauti.

 

RAYVANNY

Ameonekana kufanya poa baada ya kubadili ladha ya muziki wake kwa kugeukia Singeli, hii ni fursa ambayo Rayvanny ameamua kusepa nayo kwa kutoa ngoma inayoitwa Miss Buza ambayo iliachiwa Machi 26 akiwa amemshirikisha mfalme wa Singeli Dulla Makabila. Ngoma hii ili-trend sana YouTube kwa kukaa namba moja kwa muda mrefu ikiwa imetazamwa na watazamaji milioni 2 kwa muda wa wiki tatu.

 

ASLAY

Kwa sasa anatamba na ngoma yake mpya ya Mchepuko ambayo imeachiwa Aprili 18 ikiwa imetazamwa na watazamaji zaidi ya laki tatu ndani ya siku tatu tangu imeachiwa japo alitulia kwa muda kidogo na si kawaida yake, lakini amerudi kwa spidi ya ajabu katika kipindi hiki cha Corona.

Hakika kwa spidi hii ya wasanii wameweza kuizidi ujanja Corona kutokana na uzuri wa kazi ambazo wanatoa na zinafanya poa kwa wakati wake.

 

MAKALA | Happyness Masunga

Leave a Comment