WATU 92 wakiwemo raia 10 wa Msumbiji walioingia nchini kupitia mpaka wa Mkenda, wilayani Songea wamewekwa karantini kwa siku 14 kuangaliwa kama wameathiriwa na #CoronaVirus.
Idadi hiyo imefikiwa kutokana na watu kuanza kupelekwa katika karantini iliyopo eneo la Peramiho, Wilaya ya Songea Vijijini kuanzia Aprili 6 hadi Aprili 27, 2020.
Katika idadi hiyo kulikuwa na mtu mmoja aliyehofiwa kuwa na maambukizi ambaye ni raia wa Tanzania.
