×

Ummy Amsimamisha Kazi Mkurugenzi Maabara ya Taifa

KUFUATIA hotuba ya Rais  John Magufuli aliyoitoa jana Mei 03, 2020, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amemwagiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo kuwasimamisha kazi, Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa ya Jamii, Dkt. Nyambura Moremi na Meneja Udhibiti wa Ubora, Jacob Lusekelo ili kupisha uchunguzi.

 

Aidha,  ameunda kamati ya wataalam wabobezi tisa kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa maabara hiyo ukiwemo mfumo mzima wa ukusanyaji na upimaji wa sampuli za Covid-19.

 

Leave a Comment