STAA wa Bongo Fleva, Alikiba, amesema taasisi yake ya Kiba Foundation itatoa msaada wa mavazi 200 ya wahudumu wa afya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona (Personal Protective Equipment – PPE) ili yawasaidie wakati wa vita hii ya dunia dhidi ya virusi hivyo hasa wanapowahudumia wagonjwa wa covid-19.
