×

Takukuru Yamnasa Kigogo Ushirika, Madalali kwa Ubadhirifu – Video

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mwanza inamshikilia Mhasibu wa AMCOS ya MHED iliyopo wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga, wafanyabiashara 13 na madalali watatu kwa makosa ya kujihusisha na vitendo vya rushwa kinyume na sheria.

 

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza, Emmanuel Stenga akizungumza na waandishi wa habari jana Ijumaa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela alitoa taarifa kuhusu ubadhirifu unaofanyika kwenye pembejeo za kilimo ambapo TAKUKURU kwa kushirikiana na Bodi ya pamba imekamata dawa za Bodi ya pamba ambazo zinauzwa kwenye baadhi ya maduka ya  wafanyabiashara wa dawa za kilimo jijini Mwanza.

 

 

 

Leave a Comment