Rais Dkt. John Magufuli amemteua Dkt. Willy Lazaro Mbunju Komba kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu(Teachers’ Service Commision-TSC). Uteuzi huo umeanza jana Mei 8, 2020. Komba ni Profesa Mshiriki wa UDOM, amechukua nafasi iliyoachwa na Oliver Mhaiki aliyemaliza muda wake.
