MSANII wa Filamu na Muziki Bongo, Hemed Suleiman amelizwa na wanaosema kuwa hana nyota ya muziki hivyo ni bora aachane nao.
Akipiga stori mbili tatu na gazeti hili, msanii huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri katika Tamthiliya ya Uhuru, alisema kuwa watu wanaongea sana kuhusu yeye bila kujua malengo aliyojiwekea.
“Kuna watu wanasema kuwa sina nyota ya muziki ndiyo maana mpaka leo bado watu hawanitambui, siyo kweli, mimi najua kuimba na nina kipaji.
“Kitu kingine lazima watu wafahamu kuwa kila mtu kwenye maisha ana malengo yake, kama wananiona naendelea kutoa ngoma wajue zinanilipa,” alisema Hemed.
Stori:Memorise Ricgard
