MAMA mzazi wa msanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ amekuja juu baada ya kuulizwa kuhusu ishu ya binti yake huyo kuonekana tena na mpenzi wake, Hunchy Huncho ambaye waliashaachana.
Akizungumza na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, mama huyo alisema, hataki kumzungumzia kijana huyo kwa sababu hayupo tayari kuingilia maisha ya watu.
“Sitaki, nasema sitaki kabisa kuzungumzia mambo ya huyo kijana. Sitaki kuingilia maisha ya watu,” alisema mama Gigy.
Wiki kadhaa zilizopita ilisambaa video mtandaoni ikimuonesha mama huyo na binti yake wakimrushia mabegi mwanaume huyo nje ya geti huku wakimtolea maneno makali ambapo kijana huyo aliibuka mtandaoni na kuomba msaada.
Hata hivyo, haikuchukua muda mrefu, wawili hao wakaonekana tena wakiwa pamoja.
STORI: MEMORISE RICHARD, DAR
