×

TFF Wahojiwa na TAKUKURU Fedha za Rais Magufuli

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) imewataka maofisa wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kuzirejesha sh. bilioni moja zilizotolewa na Rais John Magufuli kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika  (Afcon) ya Vijana chini ya miaka 17 yaliyofanyika mwaka jana hapa nchini.

 

Hatua hiyo imekuja baada ya Takukuru kudai Shirikisho limekuwa na matumizi mabaya ya fedha zikiwemo fedha hizo zilizotolewa na rais. 

 

Akizungumza na vyombo vya habari leo katika ofisi za taasisi hiyo zilizopo Upanga jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Brig. John Mbungo amesema taasisi hiyo imeamuru maofisa hao wa TFF kurudisha fedha hizo kabla hatua nyingine hazijafata baada ya kupata ushahidi wa nyaraka mbalimbali.

 

Amesema wanajiandaa kuwahoji baadhi ya maofisa wa TFF kwa matumizi mabaya ya fedha ikiwemo fedha zikiwemo sh. hizo billioni zilizotolewa kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo.

 

“Kuna baadhi ya maofisa wengine wa TFF wamehojiwa na baadhi ya nyaraka zimechukuliwa na wale waliobainika kuchukua fedha hizo wana hiari ya kuzirejesha kabla ya hatua za kisheria kuchukuliwa,” alidokeza.

 

Leave a Comment