
Rais Magufuli amesema kuanzia wiki ijayo kama maambukizi ya Corona yataendelea kupungua, atafikiria kufungua Vyuo na kuruhusu michezo iendelee.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo wakati akitoa salamu baada ya kushiriki kwenye Kanisa la KKKT Chato, mkoani Geita, ambapo atafikia uamuzi wa kurejesha michezo kwa kuwa michezo ni burudani kwa Watanzania.
