×

Polepole: Uchaguzi wa 2015 Tulichelewa Kuwakata, Mwaka Huu Mapema – Video

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, chama hicho kilichelewa kuwaengua baadhi ya wanachama wake walioonekana kukivuruga na kukigawa chama hicho kwa maslahi yao binafsi lakini katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020, chama hicho kitawaengua mapema.

 

Polepole ametoa kauli hiyo leo Jumatatu, Mei 25, 2020 wakati akifanya mahojiano katika kipindi cha front Page cha +255 Global Radio.

 

“Katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, tuliona CCM kinapendwa sana na Watanzania, na wao ndio wanaweza kukielezea vizuri, na hii imetusaidia Chama tunaposimamia haki na kudhibiti viongozi wasiofuata utaratibu, tukiteua mgombea tukatoka nje huwa tunakwenda kuhalalisha tu.

“Mwaka 2015, tulichelewa sana kuwaondoa wasiofuata taratibu za chama, hawa walikuwa wakikigawa chama chetu, lakini kwa sasa CCM tumeshaweka mikakati madhubuti, wahalifu wote wamedihitiwa ipasavyo hawawezi kujitokeza tena katika uchaguzi ujao.

 

“Walioanza kujipitisha kwenye majimbo na kukusanya watu kufanya vikao au kutoa rushwa, hao tayari ‘vichwa vyao vimeliwa,’ mwaka huu CCM tumeweka mfumo madhubuti wa kupokea taarifa kwa walioanza kampeni mapema kinyume cha taratibu, hawa hawatapitishwa kamwe na CCM.

Kuhusu Mbowe kujikarantini na wabunge wenzake….

“Sote kama Taifa tupo mapambano dhidi ya Corona mpaka akina mama lishe, Freeman Mbowe na wenzake ni akina nani mpaka wawe special? Unakataza wenzako kwenda kutunga sheria Bungeni, kuungana na Watanzania ktk mapambano haya, unakula Tsh mil. 2 unakwenda kujikarantini.

 

Swali la Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko kwa Polepole.

“Katika Ilani ya CCM mwaka 2015 walisema watatenga ekari hadi milioni 5 kwa ajili ya wafugaji. Kujenga malambo 624, meli tano za uvuvi Bahari Kuu, kujenga bandari ya uvuvi, Uwanja wa Ndege Mwanza kuwa wa Kimataifa, mpaka sasa ni ndege gani ya Kimataifa inatua Mwanza?, Mhe. Polepole naomba ajibu.” – Mbunge Matiko.

Mjibu ya Polepole.

“Mwanza kule tumejenga Meli ya Mv. Vioctoria, ukiingia ndani ni kama Titanic, haijaanza safari zake kwa sababu ya janga la corona, wanaotakiwa kui-certify ianze safari zake ni Wakorea ambao ndio wameijenga, tumejenga Meli ya Umoja na meli nyingine bado zinajengwa.

 

“Mwanza ndio uwanja mrefu zaidi kwa sasa Tanzania, kama Mhe. Matiko anataka kujua ndege ya kimataifa zinazotua pale, juzi imetua ndege ya RwandAir kutoka Rwanda ikachukua minofu ya samaki na kupeleka Ulaya, usingekuwa Uwanja wa Kimataifa ndege hizo zisingetua pale.

 

Kuhusu tuhuma za kuwanunua wapinzani wahamie CCM

“Dkt. Mollel alisema nipo Chadema lakini sio chama sahihi, ni bora nirudi kwenye udaktari nikatibu watu, tukamkaribisha, hapo utasemaje amenunuliwa? Alipofika CCM ni busara kubwa ya viongozi wa Chama ilitumika kufanya maamuzi ya kumpa dhamana ya kugombea kwa tiketi ya CCM.” –

 

“Chadema nakiita Chama cha Mbowe kwa sababu sio chama hicho ni kikundi chake tu, kuna siku nilimsikia akimwambia mtu mmoja kwamba ‘be careful brother, this is my property’, maana yake ni mali yake.

Kuhusu misimamo ya Polepole

“Kuna kauli mbili ambazo nilizikemea; 1.Nape Nnauye namheshimu, alizungumzia ‘bao la mkono’ nikasema hiyo si kauli ya kiuongozi, 2.Tundu Lissu alisema ‘uchaguzi ukiwa huru na wa haki’ mshindi chama chao, vinginevyo watakwenda Ikulu kwa nguvu ya umma, huu ni uchochezi.

 

Kuhusu viwanda

“Wewe kama baba yako ameajiriwa kwenye taasisi kubwa usimdharau anayeshona kwa cherehani, fahamu kwamba hata cherehani inaingia kwenye tafsiri ya enterprises, vipo viwanda vidogo kabisa (micro enterprises), vidogo, vya kati na vikubwa. Acha dharau brother.”

 

🔴#LIVE: POLEPOLE – “TUKIFANYA UZEMBE, CCM Tunazalisha UPINZANI, CHADEMA ni CHAMA cha MBOWE”

Leave a Comment