×

Mume Amzika Mkewe Kimya Kimya, Maiti Yafukuliwa, Ndugu Waanika Mazito – Video

Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanaume aliyetambulika kwa jina la Sultan Mohamed ana shikiliwa na Jeshi la Polisi baada yakufiwa na mkewe na kuamua kumzika kimya kimya katika mazingira yenye utata kiasi cha kujengeka hisia kuwa ameuawa.

Tukio hilo lililovuta hisia za watu wengi, limejiri katika Kijiji cha Mkiu, Mkuranga mkoani Pwani na kuleta hali ya sintofahamu, iliyosababisha mwili wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Coletha Michael, ufukuliwe chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi huku mwanaume huyo akishikiliwa kwa mahojiano zaidi.

 

Global TV Online inayo habari kamili

Leave a Comment