
MHAMASISHAJI maarufu Afrika Mashariki na Kati ambaye pia ni mjasiriamali na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo, leo ameendelea na darasa lake la kuwafungua Watanzania kuhusu fursa mbalimbali za kuyafikia mafanikio yao.
Kupitia kipindi chake cha #Darasa kinachoruka kila Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 10:00 jioni hadi saa 11:00, Shigongo amesema haya;
“Dunia imebadilika sana, iwe ni kilimo, mawasiliano, hili lazima tukubaliane, watu wanaofanikiwa ni wale wanaokubalia kwenda na mabadiliko ya teknolojia, ukikataa kubadilika lazima utaachwa. Ujio wa internet ndio umeleta mabadiliko haya.
“Mtu mwenye followers elfu 20 Instagram ana nguvu, anaweza kushawishi na kufanya biashara mtandaoni, leo kuna watu wana maduka yao instagram na Facebook, wanatengeneza pesa nyingi kuliko hata wenye frame zao.
“Sayansi na teknolojia zimebadilisha kila kitu, unaweza kukuta mtu hana duka wala bidhaa lakini anakwenda kwa mwenye duka anapiga picha zile bidhaa anaposti kwenye Instagram yake kisha anaongeza asilimia 10 (faida), anauza na kupiga pesa.
“Kuna fedha nyingi sana mtandaoni kwa sababu kuna watu wengi sana mtandaoni kuliko uraiani, kitu kinachoitwa #SmartPhone kimefanya benki zinapagawa kwa sababu unafanya biashara online na unalipwa huko huko mtandaoni hata kama mteja yupo Marekani.

1. Fungua duka mtandaoni… Duka la mtandaoni halihitaji kibanda wala gharama nyingi. Tengeneza jina lako mtandaoni anza kuweka bidhaa zako taratibu, hakikisha ukurasa wako unajulikana, tumia marafiki zako kusambaza link kutangaza page yako.
“Cha msingi uwe na bidhaa zinazohitajika, lakini kama huna bidhaa unaweza kukuza page yako kisha unawafuata wenye bidhaa, unakubaliana na mwenye duka la simu anakupunguzia asilimia kadhaa, unapiga picha halafu unaanza kutangaza na kuuza kupitia page yako.
“Ukipoteza mali uliyoipata katika utafutaji iwe kwa ajali au namna yoyote sio mwisho wa mafanikio kwa sababu mafanikio yako yapo kwenye ubongo wako, ukipoteza usikate tamaa, simama, tafuta tena utapata kingi kuliko ulichopoteza,” amesema Shigongo.
“Sasa hivi #Smartphone sio kitu ambacho ni luxury, ni kifaa kinachoweza kukuingizia pesa mpaka ukashangaa, mfano una-followers milioni 7, unaweka post ya tangazo moja kwake unamlipa Tsh laki 5, kwa wiki anatengeneza pesa nyingi sana.” ameongeza mwalimu Rodrick Nabe.