
NI Sawa kusema kuwa mashabiki wa Yanga wametisha baada ya kukomba shilingi laki mbili kutoka katika droo ya tatu ya Jishindie Gari na Championi ambayo imefanyika leo Ijumaa katika Ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza Mori, Dar.
Mashabiki hao wa Yanga ambao walijitambulisha wenyewe baada ya kupigiwa simu ni Jumanne Shaban wa Manzese Dar, Mhando M. Mhano wa Tanga, Andrew Mbaya wa Dar na Amos J Paul wa Dar wao walijinasibu wazi kuwa wao ni mashabiki wa damu wa klabu ya Yanga.

Washindi wengine ni Fadhil Salum na Tanzan Shams wote wametokea Dar na wote watazawadia shilingi 50,000 kwa kila mmoja pamoja na tisheti zenye nembo ya Bahati nasibu hiyo.
Mchakato wa kuechezesha droo uliendeshwa na Idara ya Masoko na Usambazi chini ya Anthony Adam, Songolo Bilali, Jimmy Haroub na Memorise Richard ambaye alikuwa anasoma majina ya washindi hao na kuwapa taarifa kwa kuwapigia simu.

Bila kusahau uwepo wa mwakilishi kutoka katika Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Elibariki Sengasenga ambaye alikuja kushuhudia sheria na utaratibu wa kuchezesaha bahati basibu hiyo unafuatwa.
Mkuu wa kitengo cha usambazaji Anthony Adam alisema kuwa washindi wote wamepewa utaratibu wa namna gani watapewa zawadi zao, ambapo zoezi hilo litafanyika kuanzia Jumatatu ijayo kwa kuwa wikiendi hii itakuwa ni nafasi yao ya kuandaa zawadi hizo.

“Tumecheza droo yetu ya tatu leo Ijumaa (jana) na tumefanikiwa kupata washindi sita ambao wote watajishindia fedha shilingi 50,000 kila mmoja pamoja na tisheti zenye nembo ya bahati nasibu hiyo.
“Washindi wote sita tumeshawapa utaratubu wa namna gani watapewa zawadi zao, wale wa Dar nafikiri watakuja hapa hapa ofisini kwetu Sinza na yule mshindi mmoja wa Tanga tutamtumia fedha yake kupitia wakala wetu aliyopo mkoani hapo.
“Hii pia ilikuwa ni droo ndogo na ya mwisho kwenye bahati nasibu yetu hii, ambapo sasa tutakuwa tunaandaa droo ya nne na ya mwisho ambayo mshindi atakabidhiwa gari mpya yenye thamani ya shilingi milioni 10,” alisema Anthony.

Kwa upande wa washindi hao walipoulizwa kuwa wanajisikiaje kushinda fedha kupitia droo ya Baba Lao, kila mmoja alizungumza namna ambavyo amezipokea kwa furaha taarifa hizo huku wengine wakionekana kuchanganyikiwa.
“Mimi nimeshinda? Siamini dada ! Kwahiyo hizo fedha nazipataje ? Ilikuwa ni maswali mfululizo kutoka kwa Amos ambaye alionekana kupagawa kabisa baada ya kupokea taarifa hizo.
Mhando wa Tanga alipoulizwa atazifanyia nini fedha hizo alijibu kuwa: “Kwa kuwa nimeshinda leo Ijumaa, basi fedha hizo nitazitumia kununulia kanzu kwa ajili ya kwenda msikitini.”

Naye Sengasenga alisema kuwa alikuja kuiwakilisha Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ili kuona kama sheria na utaratibu unafuatwa na kuongeza kuwa amefurahishwa na namna ambavyo washindi wanapatikana kwa haki.
“Nimekuja kuangalia kama utaratubu unafuatwa wa kuchezeshwa michezo ya kubahatisha na nimefurahi kuona haki inatendeka na washindi wanapatikana kwa haki, nishauri watu wote ambao huwa wanafanya michezo hii kufuata utaratibu na sheria,” alisema Sengasenga.
Uchezeshwaji wa droo hiyo ulifanyika moja kwa moja kupitia Global Tv Online na itapatikana pia katika vituo cha Chaneli ten na mitandao yote ya Global.

Kwa kukumbusha ni kwamba kampuni ya Global Publishers ilianzisha bahati nasibu ya Jishindie Gari na Championi, ambayo ililenge kurudisha kidogo kinachopatikana kwa jamii, ambapo kupitia magazeti yao mbalimbali likiwemo Championi, wasomaji wake wanaweza kushinda zawadi mbalimbali.
Ambapo kupitia bahati nasibu hiyo, kuna gari mpya aina ya Toyota FunCargo lenye thamani ya milioni 10, litatolewa kwa mshindi wa jumla.
Hakuna gharama nyingine ambayo itafanya mtu awe mshindi zaidi ya kununua gazeti la Championi kwa shilingi 800 na kujaza kuponi iliyopo katika ukurasa wa pili na kisha kuponi hiyo ukamkabidhi wakala yeyote wa Championi au Global Publishers kwa ajili ya kuipeleka sehemu husika

JINSI YA KUSHIRIKI
Nunua Gazeti la Championi, kisha fungua ukurasa wa pili ambapo utakutana na kuponi yenye maelekezo ya kushiriki bahati nasibu hiyo. Jaza kuponi kama maelekezo yalivyo.
JINSI YA KUTUMA:
Mpe kuponi yako muuza magazeti aliye karibu nawe popote ulipo, au peleka kwenye Ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza Mori, Dar, au tuma kwa njia ya barua, Jishindie Gari, Global Publishers, S.L.P 7534, Dar es Salaam.
MASHARTI YA KUSHIRIKI:
Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd na watoto chini ya miaka 18 hawaruhusiwi kushiriki bahati nasibu hii.
Kuponi zitumwe kutoka nakala halisi ya gazeti, vivuli (fotokopi) haviruhusiwi. Mtu anaruhusiwa kutuma kuponi nyingi kadiri awezavyo ili ajiongezee nafasi ya kushinda. Kuponi zote zitachezeshwa kwenye droo ya awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu.
Issa Liponda