×

Msigwa Azungumzia Urais, Kumuachia Jimbo Steve Nyerere

MBUNGE wa Iringa Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa, baada ya kueleza kuwa anayo nia ya kugombea nafasi ya urais ndani ya chama chake, amepata kigugumizi kulijibu swali iwapo kufanya hivyo kutamfanya aachane na uwakilishi wa wananchi wake.

 

“Ni kweli nimepeleka barua siku ya jana, mimi sijasema kwamba nataka kuwaaga wananchi wa Iringa; hayo ni maneno yako.., Halafu ukisema nataka kumkimbia Steve Nyerere kwani yeye ni nani?  Na ndani ya siku nne nitaongea na vyombo vya habari kueleza kwa nini naitaka nafasi hiyo,” amesema.

 

Juni 3, 2020 Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, alitangaza rasmi kufungua mlango kwa watia nia ya kugombea nafasi ya urais katika chama hichyo, waanze kupeleka barua ofisini kwake, zoezi ambalo litahitimishwa Juni 15, 2020.

Leave a Comment