
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Hashim Rungwe, Juni 6, 2020 ametangaza chama chake kushiriki uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Akizungumza na wanahabari ofisini kwake Kijitonyama Dar, akiwa na viongozi wengine wa chama hicho Rungwe aliwaomba wafadhili wajitokeze kukifadhili chama chake ili kuweza kupata fedha za kufanyia kampeni.

Akiomba wafadhili kujitokeza alitoa akaunti namba za benki pamoja namba za simu kwa mtu anayehitaji kuwachangia kwa njia ya simu.
Alizitaja namba hizo za simu kuwa ni 0713933488, 0715387370 na 0659929882.
Katika mkutano huo Katibu wachama hicho taifa, Ali Omari ametangaza nia ya kugombea Urais wa Zanzibar mwaka huu.

HABARI/PICHA:RICHARD BUKOS /GPL