
RAPA aliyeibuliwa kwenye Bongo Star Search (BSS), Kala Jeremiah, ametoa sababu ambazo zimefanya amsifu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli kwenye mkwaju wake mpya wa Rafiki ambao unatesa kinoma mtaani.
Kala amesema Rais Magufuli ana haki ya kupewa sifa lukuki kwa sababu ameinyoosha na kuibadilisha nchi ndani ya muda mfupi.
Rapa huyo aliyasema hayo hivi karibuni wakati akihojiwa katika Kipindi cha Bongo 255 kinachobamba kupitia spika za redio bora ya mtandaoni ya +255 Global Radio kinachoruka kila Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 6 mchana hadi 10 jioni chini ya nahodha, Stewart George na mtoto mzuri, Lady T.
“Hakuna binadamu ambaye amekamilika, ila nimetoa wimbo wa kumsifu Magufuli kwa sababu nimeona amefanya mazuri mengi, hakuna mtu ambaye anaweza akampinga kwa haya aliyoyafanya ndani ya muda mfupi,” alisema Kala.
Hivi karibuni, Kala alitimba Studio za +255 Global Radio kuutambulisha wimbo huo na kuwashukuru mashabiki wake ambao siku zote wamekuwa wakimpa moyo wa kuendelea kufanya kazi nzuri, lakini pia aliishukuru Global Publishers kwa kumpa sapoti katika kuufikisha muziki wake mbali.
Ili kusikiliza matangazo ya +255 Global Radio popote ulipo, pakua App ya Gobal Radio katika Android au iOS au ingia www.globalradio.co.tz.