×

‘Mpemba wa Magufuli’ na Wenzake Watakiwa Kupelekwa Mahakamani

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewataka washtakiwa katika kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili mfanyabiashara, Yusufu Ali maarufu ‘Mpemba wa Magufuli’ na wenzake  wanatakiwa kupelekwa mahakamani hapo ili kesi hiyo iweze kuendelea kwani shauri hilo limesimama kwa muda mrefu.

 

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka manne ya kujihusisha na biashara ya Meno ya Tembo yenye thamani ya Sh 785.6 milioni. Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba amesema itatolewa gari ya kuwatoa mahabusu ili kesi iweze kuendelea.

Awali Wakili wa Serikali, Kija Luzingana ameidai kuwa hawawezi kundelea na usikilizwaji kutokana washtakiwa hao hawawezi kufikishwa mahakamani hapo kutokana na ugonjwa wa corona.

 

Kesi hiyo, imeahirishwa hadi Juni 12, 2020 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi. Mbali na Ali washitakiwa wengine ni Charles Mrutu, Benedict Kungwa, Jumanne Chima, Ahmed Nyagongo na Pius Kulagwa.

Leave a Comment