×

Uchumi wa Tanzania Kukua kwa Asilimia 5.5 Mwaka 2020 – Video

WAZIRI  wa Fedha Dk Philip Mpango, amesema kasi ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania inatarajiwa kupungua kidogo hadi asilimia 5.5 mwaka 2020 kutoka kwenye maokeo ya awali ya asilimia 6.9.

 

“Mwaka 2019, Pato la Taifa kwa bei za miaka husika lilikuwa shilingi trilioni 139.9 ikilinganishwa na shilingi trilioni 129.0 mwaka 2018..

 

“Kwa mwaka 2020 ukuaji wa pato la taifa unatarajiwa kupungua kidogo kutoka kwenye maoteo ya awali ya asilimia 6.9 hadi asilimia 5.5 kutokana na hatua madhubuti zilizochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais John Magufuli na hususan kuhimiza wananchi waendelee kufanya kazi wakati wanaendelea kuchukua tahadhari dhidi ya corona kama ilivyoelekezwa na wataalamu wa wa afya pamoja na matarajio ya kuimarika kwa uchumi wa kikanda na dunia.

 

“Serikali imenunua ndege mpya 11. Kati ya hizo, nane (8) zenye thamani ya Sh. 1.27 trilioni na tayari malipo ya awali ya Sh. 85.7 bilioni kwa ajili ya ununuzi wa ndege nyingine mpya tatu (3) yamefanyika.

 

“Hadi Aprili 2020, deni la Serikali lilifikia Sh. 55.43 trilioni. Kati ya kiasi hicho, deni la nje lilikuwa Sh. 40.57 trilioni na deni la ndani Sh. 14.85 trilioni. Ukuzaji rasilimali kwa bei za miaka husika ulifikia Sh. 55.5 trilioni mwaka 2019 ikiwa ni ongezeko la asilimia 12.1 ikilinganishwa na Sh. 49.5 trilioni mwaka 2018.

 

“Tanzania Bara ilikadiriwa kuwa na watu 54,265,158 mwaka 2019 ikilinganishwa na watu 52,619,314 mwaka 2018. Pato la wastani la mtu kwa mwaka 2019 lilikuwa Sh. 2,577,967, ikilinganishwa na Sh. 2,452,406 kwa 2018.

 

“Thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya sarafu kubwa duniani imekuwa tulivu kwa 2019/20. Katika kipindi cha Julai 2019 hadi Aprili 2020, dola moja ya Marekani ilibadilishwa kati ya Sh. 2,299.3 na Sh. 2,302.7. Hadi Aprili 2020 akiba ya fedha za kigeni ilifikia Dola za Marekani bilioni 5.3 kiasi kinachotosha kulipia biadhaa kutoka nje ya nchi kwa miezi sita.

 

“Nimpongeze kwa dhati Rais Magufuli, kwa jinsi anavyoliongoza Taifa kwa kipindi cha miaka 4 ya utawala wake, tumeshuhudia kuimarika kwa bei, kipekee nimshukuru pia kwa kuniamini kuongoza Wizara ya Fedha na tangu mwanzo hadi sasa,” Dkt. Mpango ameliambia Bunge Alhamisi, Juni 11, 2020.

 

Hata hivyo, matarajio hayo mapya yapo juu kidogo kutoka yale ya awali yaliyokuwa yamebainishwa na Dk Mpango wakati akisoma bajeti ya wizara yake.

 

Leave a Comment