
Bunge la Tanzania limepitisha bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2020/21. Jumla ya kura zilizopigwa ni 371, Kura za Ndio 304. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anahutubia kuhitimisha Bunge la 19 leo huku Rais Dkt John Magufuli akitarajiwa kuhutubia na kulivunja bunge hapo kesho.
“Sitosahau tukio la Novemba 19, 2015, siku ambayo Rais Magufuli alipowasilisha jina langu ktk Bunge lako Tukufu na kupendekeza niwe Waziri Mkuu, nawashukuru kwa imani mliyoionesha kwa kuridhia mapendekezo hayo na kunipigia kura za ndiyo.
“Tumeshughulikia nidhamu ya watumishi wa umma, mapambano dhidi ya rushwa ndani na nje ya Serikali, hii itakuwa endelevu kung’oa kabisa rushwa nchini, yumeimarisha vyombo vya ulinzi na usalama. Tunaendelea kupambana na wanaojihusiosha na biashara ya madwa ya kulevya.
“Tumezidi kuimarisha mazao muhimu kama korosho, huduma za pembejeo na huduma za ugani. Kuanzisha masoko ya madini maeneo ya migodi ili kuongeza mapato ya Serikali, kuhamishia makao makuu Dodoma, sasa watumishi wote wapo Dodoma na shughuli zinaendelea.
“Tumeimarisha sekta ya elimu, sekta ya afya kwa kujenga zahanati, hospitali za wilaya, za rufaa, za kanda na kuongeza madawa na vifaa tiba. Miradi ya maji mijini na vijijini. Zoezi ya kupeleka maji katika vijiji vyote bado linaendelea.
“Tumeweza kuokoa Bil 19.83 kwa kuwaondoa kwenye mfumo wa malipo, watumishi hewa zaidi ya elfu 19, na wenye vyeti vya kughushi 15,411, masuala ya uhakiki watumishi hewa, yanaendelea kwenye Wizara zetu.
“Kwa mujibu wa taarifa za Taasisi ya Global Peace Index 2020 inayofuatilia masuala ya amani Duniani, Tanzania ni nchi ya saba Afrika na ya kwanza Afrika Mashariki kwa kuwa na amani na utumivu.
“Tumenunua ndege 11 za ACTL ambazo baadhi yake tayari zimeshaanza safari za ndani na nje ya tanzania, tumejenga meli na zimeshaanza kufanya kazi Ziwa Tanganyika na Ziwa Victoria, vivuko, barabara, madaraja, mradi wa Umeme wa Nyerere (Stiegler’s), miradi ya maji.
“Mhe. Spika, Serikali ya CCM kupitia Bunge lako Tukufu kwa kipindi cha miaka mitano, imeidhinisha kiasi cha Tsh tril 126.8 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kote nchini, Watanzania mmeshuhudia miradi yote hiyo.
“Maambukizi na wagonjwa wa Corona wamepungua Hospitalini, anayestahili sifa ni Rais Magufuli kwa msimamo na maono yake yalikuwa chachu ya kupunguza ugonjwa huo, ameifanya Tanzania kuwa ya mfano wa kuigwa Duniani kwa namna alivyoshughulikia ugonjwa huu.
“Kwa taarifa ya leo mpaka mchana, kutoka katika vituo vya kutolea huduma vya Serikali na Binafsi wagonjwa wa Corona nchini wamebaki 66 katika Mikoa 10, katika Mikoa 16 haina wagonjwa, mikoa hiyo ni Arusha, Dodoma, Geita, Kagera, Katavi, Kigoma, Lindi, Mara, Mtwara, Manyara, Pwani, Rukwa, Ruvuma, Simiyu, Songwe na Tabora.
“Tumefanikiwa kuimarisha uwekezaji wa kujenga viwanda, hadi Aprili 2020, jumla ya viwanda vipya 8,477 vikiwemo vidogo, vya kati na vikubwa vimeanzishwa na kupelekea ajira za viwandani kufikia 482,601.” amesema Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.