×

Mahaba ya Nandy, Harmo Yamtishia Amani Sarah

WAKATI wimbo wao mpya wa Acha Lizame ukiendelea kutikisa kwenye mitandao ya kijamii, redioni na televisheni, picha za kimahaba walizopiga wanamuziki wa Bongo Fleva, Faustina Charles ‘Nandy’ na Rajab Abdul ‘Harmonize’ zimeibua msala, Gazeti la IJUMAA WIKIENDA limenasa mchapo mpya, karibu!

 

TUJIUNGE NA CHANZO

Chanzo makini kimeeleza kuwa, picha hizo zimezua msala pande zote mbili, kwani mpenzi wa Nandy; William Lymo ‘Billnass’ hakufurahishwa na picha hizo za kimahaba walizopiga, huku upande wa pili, mke wa Harmonize au Harmo; Sarah Michelotti, naye akicharuka kama kawaida yake.

 

“Unajua ishu ni kwamba, kila mmoja alimuaga mpenzi wake kwenda kupiga picha hizo hususan wakati ule wa kurekodi video, lakini sasa kilicholeta utata ni kule kubusiana huku wengine wakienda mbali zaidi kwa kupeleka maneno ya umbea kwa wahusika,” kilisema chanzo hicho makini.

WAMBEA WATAJWA

Chanzo hicho makini kiliongeza kuwa, wambea wasiopenda mambo ya watu, ndiyo waliojiongeza kwenda kumueleza Billnass au Bilinenga kuwa mbali na kushuti, kuna mengine waliyafanya nje ya wimbo ambayo ndiyo yalimfanya Billnass ‘amaindi’.

 

Lakini kama hiyo haitoshi, chanzo hicho kinaeleza kuwa, kilichochangia kuwachanganya zaidi Billnass na Sarah, ni mitandao ya kijamii, kwani ndiyo iliyokata picha hizo na kuzisambaza huku wakieleza kwamba kuna zaidi ya ‘shooting’.

 

IJUMAA LASHUHUDIA

Gazeti la IJUMAA WIKIENDA liliingia kwenye ‘pages’ mbalimbali za mitandao ya kijamii na kushuhudia maneno kama yote ambapo mjadala zaidi ulikuwa ni kwenye picha hizo na jinsi wawili hao walivyooneshana mahaba.

 

“Mh! Haiwezekani mtu sio mpenzi wako halafu mbusiane kwa staili hii? Hawa wamefanya yao tu.”

“Harmo kama Harmo, mshuti video kama hii halafu akuache hivihivi, unamjua au unamsikia?”

 

“Hii hata kama ni kazi, lakini hawa wamepitiliza. Si bure itakuwa walijiongeza wakaburudika nyuma ya kamera.”

Hayo yalikuwa ni baadhi ya maoni mbalimbali yaliyokuwa yanatrendi kwenye mitandao ya kijamii hususan Instagram katika ‘pages’ nyingi za kidaku.

 

WENYEWE WANASEMAJE?

Gazeti la IJUMAA WIKIENDA lilifanya jitahada za kuwatafuta Billnass na Sarah ambao wanadaiwa kuibiwa mali zao, lakini hata hivyo hawakupatikana na kutoa ushirikiano mzuri.

 

TUMSIKIE NANDY…

Hata hivyo, Gazeti la IJUMAA WIKIENDA lilifanikiwa kumpata Nandy ambaye pamoja na mambo mengine, alizungumzia picha hizo na kusema zimekuzwa zaidi na watu wa mitandaoni, lakini kwao hawakuona kama ni tatizo.

 

“Unajua tena mashabiki, lazima waseme hayo mambo, lakini sisi tulitambua tunachokifanya. Kila mtu pale alikuwa kazini na hakuna cha ziada,” alisema Nandy.

 

AWASHUKURU WATANZANIA

Mrembo huyo pia alieleza kuwa, anawashukuru Watanzania kwa kumuunga mkono kwani wimbo huo umepata mafanikio makubwa ndani ya muda mfupi tofauti na alivyotarajia.

 

“Video tumefanya hapahapa ndani (nchini), imetumia pesa fulani hivi ndefu, lakini nisingependa kuzianika, lakini kiukweli mimi mwenyewe nimeishangaa namna ambavyo imepokelewa kwa ukubwa,” alisema nandy na kuongeza;

 

“Wakati tunashuti, kwa kweli sikutegemea kama inaweza kuwa bora kwa kiasi hiki ambacho nimekuja kukiona baada ya kuachiwa rasmi.”

 

PICHA ZENYEWE

Picha hizo zilizozua balaa zimepigwa wakati Nandy alipokuwa anashuti video ya wimbo wake huo unaokwenda kwa jina la Acha Lizame ambao amemshirikisha Harmo.

 

Wimbo huo ulioachiwa Ijumaa iliyopita, mpaka juzi Jumamosi, tayari ulikuwa namba mbili kwenye trending YouTube ukiwa umetazamwa na zaidi ya watu laki nne kuelekea laki tano ndani ya saa 24 (siku moja).

Wimbo huo unatabiriwa kuwa utaweka rekodi mbalimbali nje na ndani ya Bongo.

STORI: MEMORISE RICHARD, DAR

Leave a Comment