
MSHAMBULIAJIwa Difaa El Jadida ya nchini Morocco, Simon Msuva, anatarajia kuipa mkono wa kwa heri timu hiyo baada ya mkataba wake wa miaka mitatu kufi kia tamati mwishoni mwa msimu huu.
Msuva alijiunga na Difaa mwaka 2017 kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Yanga aliyoitumikia kwa muda wa miaka sita ambayo aliichezea kwa mafanikio makubwa.
Akizungumza na Championi Jumatano,baba mzazi wa Msuva, Happygod Msuva, amefunguka kuwa, mwanaye huyo ana asilimia chache ya kubaki katika klabu yake hiyo ya El Jadida baada ya mkataba wake kufi kia tamati mwishoni mwa msimu huu.

“Msuva tayari ameshamaliza mkataba wake na El Jadida, mwezi wa nane anatarajia kurudi Bongo, kuna asilimia ndogo ya kuweza kuendelea kubaki katika klabu hiyo kwa kuwa kuna mipango yake mingine anaifanya.
“Kuna mazungumzo na timu mbalimbali ambayo anayafanya kwa sasa na mambo yatakapokamilika kila kitu kitakuwa hadharani na kujua wapi atakwenda lakini kwa asilimia kubwa ana nafasi ndogo ya kubaki El Jadida.
“Kwa sasa bado yupo huko kutokana na ligi ya nchini humo kutofunguliwa ambapo inatarajia kufunguliwa mwezi ujao,” alisema mzee Msuva.
Stori: Khadija Mngwai, Dar es Salaam