×

Mil 40 Zamshusha Mnyarwanda Yanga

LICHA ya beki wa kushoto, Eric Rutanga ambaye anawaniwa na Yanga kusaini mkataba na Polisi Rwanda FC, imebainika kuwa hilo haliwezi kumzuia beki huyo kuvaa uzi wa Jangwani kwa msimu ujao.

 

Hiyo imekuja baada ya kuvuja kwa taarifa kuwa kuna kipengele ambacho kinamruhusu beki huyo kutua sehemu yoyote kwa klabu ambayo itakuwa tayari kulipa kiasi cha fedha za Rwanda milioni 15 (sawa na mil 36 za Kitanzania), ambazo alichukua kabla ya kusaini klabu hiyo.

 

Chanzo cha karibu na beki huyo kimeliambia Championi Jumatano, kuwa mkataba huo haumzuii Rutanga kwenda Yanga kwa sababu ya kipengele hicho cha kuondoka klabuni hapo muda wowote ikitokea timu ambayo itakuwa na uwezo wa kulipa fedha hizo.

 

“Unajua licha ya kwamba Rutanga amesaini Polisi Rwanda akitokea Rayon Sports lakini pia anaweza kutua Yanga kama watakuwa na nia hiyo ya kutaka kumsajili kwa msimu ujao.

 

“Ni kwamba licha ya kusaini mkataba huo na Polisi, kuna kipengele ambacho kinamruhusu yeye kutua kwenye klabu yoyote ile ambayo itakuwa tayari kulipa kiasi kile ambacho amekichukua Polisi.

 

“Kiasi hicho ni mil 15,000,000 za hapa Rwanda sawa na mil 36,142,200 za Tanzania, kwa hiyo kama wakiwa na zaidi ya mil 40 basi wanaweza kabisa kumsajili wao kama ambavyo walikuwa wanamfuatilia tangu awali,” kilisema chanzo hicho.

Stori na Said Ally, Dar es Salaam

Leave a Comment