×

Corona Yaleta Baraka Kwenye Sekta Ya Afya – Ummy Mwalimu

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto amesema ugonjwa wa Corona umeleta fursa ya kuboresha huduma za afya kwani michango mbalimbali iliyotolewa imesaidia kuokoa maisha ya wagonjwa mahututi.

Waziri Ummy Mwalimu ameyasema hayo wakati anazindua upanuzi wa wodi ya hospitali ya Ibrahimu Haji itakayotumika kwa ajili ya kina mama na pia kufungua rasmi huduma za magonjwa  ya kawaida ambapo hapo awali walikuwa wakihudumia wagonjwa wa Corona tu.

“Tunaishukuru Jumuiya ya Khoja Shia Ithna Asheri Jamaat ambao ndio wamiliki wa hospitali hii kwa kujitoa kwao wakati wa kipindi cha ugonjwa wa Corona. Mlituletea msaada wa chakula na kwa niaba ya serikali tunashukuru na tunathamini mchango wenu,” alisema Waziri huyo wa Afya.

Waziri huyo amezindua rasmi hospitali hiyo huku ugonjwa wa Corona ukiwa umepungua sana huku akisisitiza wanachi kuendelea kuchukua tahadhari.

Leave a Comment