
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kiungani iliyopo Kurasini Wilayani Temeke, Dar wamerejewa na furaha baada ya kutatuliwa tatizo lao la kukosa choo muda mrefu jambo lililokuwalikisababisha adha kubwa katika taaluma.
Baada ya kilio hicho kampuni ya mafuta ya Vivo Energy Tanzania imesikia kilio chao na kuwakarabatia jengo la choo chao cha zamani na kulifanya liwe la kisasa likiwa na matundu 16.

Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi choo hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa Vivo Energy Tanzania Mohamed Bougriba amesema wanayofuraha kubwa kwa kuona wanarudisha wa jamii sehemu ya wanachokipa kutoka kwa jamii. Ambapo aliendelea kusema;
“Kama Vivo Energy leo tunajisikia furaha kubwa sana kushirikiana na jamii haswa walimu na wanafunzi wa shule hii kwa kuwapa msaada huu wa kutukarabatia choo chet na kuwa cha kisasa hivyo kupunguza adha waliyokuwa nayo hapo awali.

“Tunaamini kwa kuwapunguzia changamoto hii kwa hiki kidogo tulichowapa inaweza kuchangia maendeleo ya shule hii na kuongeza ufanisi kwa wanafunzi.” Alimaliza kusema.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bonivilia Malya aliipongeza Kampuni ya Vivo Energy kwa kuiangazia shule hiyo kwa msaada huo utakaomaliza uhaba wa vyoo salama na kisasa.

Msaada huu umekuja sehemu muafaka ambapo hapo awali tulikuwa na changamoto ya vyoo bora na vya kisasa lakini kwa msaada wa wenzetu wa Vivo Energy sasa nasi wanafunzi wetu watakuwa wanatumia choo safi na salama cha kisasa.
Kwa kumalizia niwaombe wadau wengine wajitokeze sehemu mbalimbali zinazohitaji misaada kama hii na kupunguza changamoto katika jamii. HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL