×

Kocha Yanga Akabidhi Mashine Mbili Majukumu

KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael, raia wa Ubelgiji, amefunguka kuwa hakutakuwa na pengo lolote la kumkosa beki wake wa kati Lamine Moro kwenye mechi atakazokuwa nje kwa sababu ana zaidi ya wachezaji wawili wa kuziba nafasi hiyo.

 

Kocha huyo ameongeza kwamba tayari ameshawaandaa Kelvin Yondani na Andrew Vincent ‘Dante’ kwa ajili ya kuziba nafasi ya beki huyo Mghana akianza na mechi yao ya jana dhidi ya Azam FC.

 

Lamine ana hatihati ya kukosekana kwa msimu wote kwa kuwa anakabiliwa na adhabu ya kufungiwa miezi mitatu hadi 12 au atafungiwa kucheza idadi ya mechi ambazo kamati ya utendaji itaona inafaa au atalipa faini ambayo itapangwa na kamati ya utendaji au vyote kwa pamoja kutokana na kosa la kumrukia kwa makusudi na kumpiga teke kiungo wa JKT Tanzania, Mwinyi Kazimoto.

Eymael ameliambia Championi Jumatatu, kuwa hakutakuwa na pengo la Lamine hata kidogo kwa sababu wachezaji Eymael azikabidhi mashine mbili… hao wawili pamoja na Ally Mtoni ‘Sonso’ wanaweza kutumika katika nafasi hiyo na kucheza vizuri.

 

“Kwanza kuhusu Lamine ni mchezaji mzuri na ambaye nimemtumia sana kwenye mechi zetu lakini naona kukosekana kwake wala haitakuwa tatizo kubwa.

 

“Nasema hivyo kwa sababu Yondani amekuwa kwenye fomu ya hali ya juu, kwa hiyo anaweza kucheza na Makapu (Said) na wakawa na muunganiko mzuri tu kwenye mechi zote ambazo tutamkosa.

 

“Lakini pia namrudisha Sonso (Ally Mtoni) katika kundi na ana uwezo wa kucheza hapo, pia usisahau kuhusiana na Dante ambaye naweza kumtumia pia. Kwa hiyo utaona kwa kiwango gani hakutakuwa na madhara ya kumkosa,” alisema Eymael.

MWANDISHI WETU,Dar es Salaam

Leave a Comment